Mgomo wa siku 56 wa madaktari katika hospitali za umma nchini Kenya, hatimaye wafikia muafaka, baada ya kufanya makubaliano na serikali siku ya Jumatano, na kutia saini mkataba wa kurejea kazini mara moja licha ya kutofikia muafaka kuhusiana na mishahara ya madaktari wanafunzi.
Rais wa Kenya William Ruto ametangaza Ijumaa wiki hii kuwa siku kuu ya kitaifa kuomboleza vifo vya watu 238 waliofariki kutokana na mafuriko.
Kenya, Uganda, Rwanda, DRC na Sudan Kusini zimeamua kuweka nguvu ya pamoja kufanikisha ujenzi wa reli ya mwendo kasi SGR inayopita Afrika Mashariki.
Kenya Jumapili imesema kwamba idadi ya vifo kutokana na mvua kali na mafuriko ya wiki kadhaa imeongezeka hadi 228 na kuonya kuwa hakuna dalili ya afueni wakati huu.
Idadi ya vifo kutokana na mafuriko nchini Kenya imevuka 200 tangu mwezi Machi, wizara ya mambo ya ndani imesema Ijumaa, huku kimbunga kikielekea pwani ya Tanzania.
Mwaka huu Sherehe za Siku ya Kimataifa ya Wafanyakazi zina hisia ya dharura ya kujitolea upya kwa haki za kijamii, wakati tunapopitia kipindi kigumu, ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa na mabadiliko ya haraka katika sehemu za kazi kutokana na maendeleo ya teknolojia.
Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways Jumatatu limesema litasitisha safari za ndege kuelekea mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Kinshasa, baada ya mamlaka ya kijeshi kushindwa kuwaachilia wafanyakazi wake inaowazuia licha ya amri ya mahakama.
Watu 42 wamefariki katika mafuriko katika eneo la Mai Mahiu katikati mwa Kenya baada ya bwawa kupasuka mapema Jumatatu, na idadi ya vifo inaweza kuongezeka, polisi wamesema.
Jeshi la Kenya lilifanya operesheni Alhamisi kuwaokoa wahanga wa mvua kubwa iliyosababisha vifo vya darzeni za watu kote Afrika Mashariki katika muda wa mwezi mmoja uliopita.
Wabunge wanane wa Uganda wako Nairobi Kenya kwa ziara ya mafunzo juu ya kushughulikia changamoto za ukuaji wa miji nchini humo ikiwemo udhibiti makazi duni na kupitisha sera mahiri za ukuaji wa miji mikubwa.
Jumla ya watu 118 walikuwa waathirika wa mauaji holela yaliyotekelezwa na polisi wa Kenya mwaka uliopita, makundi ya haki za binadamu ya ndani na ya kimataifa yamesema katika ripoti iliyochapishwa Jumatano, yakilaani “kutowajibishwa” kwa maafisa wa usalama waliohusika katika mauaji hayo.
Kenya imetoa tahadhari ya mafuriko wakati mvua kubwa zikinyesha katika eneo hilo. Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya limesema mafuriko katika taifa hilo la Afrika Mashariki yameua watu 38 na zaidi ya 11,000 wamekoseshwa makazi.
Pandisha zaidi