Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 03, 2024 Local time: 21:39

Mvua nyingi zina sababisha mafurikiko Afrika Mashariki


Mafuriko katika eneo la kijiji cha Ombaka , Kisumu, Kenya, Aprili 17, 2024.Picna na AP
Mafuriko katika eneo la kijiji cha Ombaka , Kisumu, Kenya, Aprili 17, 2024.Picna na AP

Mafuriko makubwa yameyakumba maeneo mengi ya Afrika Mashariki ambayo yanakabiliwa na mvua za mfululizo, Burundi ikiomba msaada wa kimataifa wa kuisaidia kupambana na maafa hayo.

Maji katika Ziwa Tanganyika yameongezeka na kusababisha mafuriko katika bandari ya Bunjumbura, biashara zimevurugika katika mji mkuu wa kiuchumi na katika maeneo mengine yanayotegemea kwa kiwango kikubwa msaada kutoka wafadhili.

Raia wa Burundi walikuwa wakihangaika kukabiliana na mafuriko baada ya mvua kubwa kunyesha nchini humo, huku maelfu ya watu wakikosa makazi na nyumba nyingi na shule kuharibiwa.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa tangu Septemba zaidi ya watu 200,000 wamekimbia makazi yao kutokana na mafuriko kufuatia hali mbaya ya hewa ya El Nino.

Serikali imetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kusaidia katika kukabiliana na hali hiyo mbaya.

Nchi za Tanzania na Kenya zimeshuhudia zaidi ya vifo 50 na maelfu kukoseshwa makazi kutokana na mafuriko yaliyoathiri kanda hiyo.

Baadhi ya habari hii inatoka shirika la habari la AP

Forum

XS
SM
MD
LG