Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 19, 2024 Local time: 21:22

Ruto aahidi kuuboresha uchumi wa Kenya


Waendesha pikipiki za “Bodaboda” Nairobi katika uzinduzi wa kituo cha kwanza cha kuchaji umeme barani Afrika, Mei 26, 2023. (Picha na SIMON MAINA / AFP)
Waendesha pikipiki za “Bodaboda” Nairobi katika uzinduzi wa kituo cha kwanza cha kuchaji umeme barani Afrika, Mei 26, 2023. (Picha na SIMON MAINA / AFP)

Rais William Ruto amefanya ahadi kadhaa wakati akitoa hotuba yake katika maadhimisho ya miaka 60 ya kumbukumbu ya siku ya Madaraka yaliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Moi katika Kaunti ya Embu.

Mkuu wa nchi aliahidi kushughulikia uanzishaji wa mfumo wa usafiri wa umeme ambayo utaona kuwa bodaboda za umeme zitaingia kwenye soko la Kenya.

Pia aliahidi kuazinsiha maeneo matano ya ziada ya uuzaji nje wa bidhaa ili kuvutia uwekezaji wa ndani na wa kimataifa.

Rais pia alielezea kwamba Chuo Kikuu cha Kenya yaani Open University, ambacho tayari kimeanzishwa, kitakuwa na hati miliki yake katika masomo kuanzia mwezi huu.

Chuo kikuu cha Kitaifa ni moja ya miradi ya serikali inayolenga kufanya elimu ya chuo kikuu kuwa ni ya gharama nafuu, inafikiwa na wengi, na kila wanafunzi wote wanafursa ya kuipata.

Rais Ruto pia ameahidi kukamilisha miradi inayoendelea ya miundo mbinu ikiwemo barabara kadhaa na mabwawa ambayo yako katika hatua za ujenzi katika Kaunti ya Embu na sehemu nyingine za nchi.

Pia ni muhimu kuelezea kwamba ujumbe wake ulikuwa na maombi mazito kwa wakenya kukumbatia Mswaada wa Fedha wa 2023 na ulea wa Ufadhili wa Nyumba.

“Ndiyo maana wapigania uhuru wanafikiria kuwa asili ya maadilini ni sababu tosha ya kutuzwa. Kwa mfano, wale ambao wanalipwa kiasi cha shilingi laki mbili za kenya watalipa tu shilingi 2,500 kufadhili mpango huo ambao utasaidia kufungua mamilioni ya nafasi za ajira kwa vijana na kuwaletea mlo mezani watu ambao maarufu amewaita mahustler. Huu ni mchango wenye tija sana kwa ajili ya hali njema, alisema..

Forum

XS
SM
MD
LG