Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 20, 2024 Local time: 05:12

Viongozi wakutana Cairo kwa juhudi za kusuluhisha mzozo wa Israeli na Hamas


Viongozi wakutana mjini Cairo, Misri, katika juhudi za kutafuta amani Mashariki ya kati. Picha na Shafi Mbinda, VOA, Misri.
Viongozi wakutana mjini Cairo, Misri, katika juhudi za kutafuta amani Mashariki ya kati. Picha na Shafi Mbinda, VOA, Misri.

Shughuli za mkutano wa kimataifa wa amani zilianza Jumamosi asubuhi mjini Cairo, Misri, ambapo viongozi wa kiserikali kutoka mataifa mbalimbali pamoja na taasisi za kimataifa walianza kujadili maendeleo na mustakabali wa mzozo wa kadhia ya wanamgambo wa Kundi la Hamas na Israeli.

Viongozi hao, ambao walianza kuwasili tangu Ijumaa jioni wanahudhuria mkutano ambao pia ulikusudiwa kuangazia kwa kina mizizi ya mzozo huo wa kihistoria kati ya Wapalestina na Waisraeli, na kusukuma mbele mchakato wa amani katika eneo la Mashariki ya Kati ili kupata suluhu ya haraka ya nchi mbili zinazotambulika kimataifa.

Nchi zisizopungua 31 zinawakilishwa na mawaziri pamoja na viongozi wengine wa kiserikali kutoka Jordan, Qatar Uingereza, Italia, Afrika ya kusini, Uhispania, Palestina, Emirates, Bahrain, Saudi Arabia, Kuwait, Iraq, Italia, Cyprus, Uturuki, Brazil, Morocco, Norway, Ugiriki na nyinginezo pamoja na uwepo wa Mjumbe Maalum wa China, Mjumbe Maalum wa Marekani, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, na

Siku ya Ijumaa Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak alikutana na Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi mjini Cairo kuonyesha msimamo nchi yake katika kushughulikia mzozo wa Israel na Palestina.

Kwenye ziara yake ya Mashariki ya Kati Sunak alielezea kuguswa na vifo vya raia kufuatia mashambulizi kati ya Israel na Ukanda wa Gaza mapema Ijumaa mjini Cairo.

Akizungumza na marais wa Misri na Palestina kwa nyakati tofauti, Sunak alitoa pole kwa rais Mahmoud Abbas ambapo kwa sasa yupo Misri akitazamiwa kuwa mmoja wa watakaohudhuria mkutano wa kimataifa wa amani uliopangwa kufanyika Jumamosi kufuatia kadhia inayoendelea katika ardhi ya Palestina.

Akizungumza na mwenyeji wake Rais Abdel Fattah El-Sisi, Sunak alipongeza "juhudi chanya za Misri pia katika mzozo unaoendelea."

Aidha alihimiza kuendeleza mawasiliano zaidi ndani ya kipindi hiki cha mzozo.

Waziri Mkuu Sunak aliweka wazi kuwa Uingereza inaamini umuhimu wa kutuma misaada kwa watu wa Palestina na kuifikisha kupitia Misri.

-Imetayarishhwa na Shafii Mbinda, Sauti ya Amerika, Cairo, Misri.

Forum

XS
SM
MD
LG