Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 20, 2024 Local time: 03:33

Uchaguzi mkuu Macedonia


Hristijan Mickoski, kiongozi wa upinzani akipiga kura katika kituo cha Skopje, North Macedonia, May 8, 2024.
Hristijan Mickoski, kiongozi wa upinzani akipiga kura katika kituo cha Skopje, North Macedonia, May 8, 2024.

Wapiga kura nchini North Macedonia wanapiga kura leo Jumatano kuwachagua wabunge, na duru ya pili ya kumchagua rais, katika uchaguzi ambao umegubikwa na maswala mengi yakiwemo dhamira ya nchi hiyo kujiunga na umoja wa ulaya, ufisadi na uchumi wa taifa.

Duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais asiyekuwa na mamlaka makubwa, ilionekana kama mtihami kwa uchaguzi wa wabunge.

Gordana Siljanovska-Davkova, anayeungwa mkono wana vyama vya upinzani, alionekana kuwa msitari wa mbele katika uchaguzi huo.

Anakabiliana na rais wa sasa Stevo Pendarovski, anayeungwa mkono na muungano wa vyama vilivyo madarakani, vya mrengo wa kushoto.

Siljanovska-Davkova alipata asilimia 41, katika raundi ya kwanza iliyofanyika April 24, ikilinganishwa na asilimia 20.5 ya kura alizopata Pendarovski.

Wawili hao walikabiliana katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2019 ambapo Pendarovski alipata ushindi wa asilimia 54.

Ni lazimia asilimia 40 ya wapiga kura washiriki duru ya pili ndipo matokeo yakubalike.

Forum

XS
SM
MD
LG