Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 20, 2024 Local time: 02:03

Taliban wameuawa katika mlipuko wa bomu Afghanistan


Waombolezaji wakiwa karibu na mwili wa mtu aliyefariki kutokana na bomu la kujitoa mhanga Kandahar, March 21, 2024.
Waombolezaji wakiwa karibu na mwili wa mtu aliyefariki kutokana na bomu la kujitoa mhanga Kandahar, March 21, 2024.

Mlipuko wa bomu katika jimbo la Badakhshan, kaskazini mashariki mwa Afghanistan, umeua maafisa wa usalama watatu na kujeruhi wengine sita.

Vyanzo kadhaa vya habari wakiwemo wakaazi wa sehemu hiyo na maafisa wa afya wamethibitisha tukio hilo.

Wamesema kwamba kilipuzi kilichokuwa kimetegwa kwenye pikipiki kililipuka wakati msafara wa Taliban ulipokuwa unapita katika mji wa Faizabad.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani Abdul Mateen Qani amethibitisha tukio hilo na kusema kwamba bomu hilo lilikuwa limewalenga maafisa wa usalama waliokuwa wanaelekea katika shughuli za kuharibu mabomu.

Qatani amesema uchunguzi unaendelea.

Hakuna kundi kufikia sasa limedai kuhusika katika sehemu hiyo ya Badakhshan ambapo kumekuwa na maandamano mabaya ya raia dhidi ya utawala wa Taliban.

Maandamano ya ijumaa yalisababisha vifo vya waandamanaji wawili baada ya kutokea makabiliano na maafisa wa usalama.

Forum

XS
SM
MD
LG