Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 04, 2024 Local time: 13:16

Mwanamuziki maarufu wa Iran ahukumiwa kifo kwa kuunga mkono maandamano


Mwanamuziki wa Iran Toomaj Salehi
Mwanamuziki wa Iran Toomaj Salehi

Mahakama ya mapinduzi ya Iran imemhukumu kifo mwanamuziki maarufu wa Iran Toomaj Salehi kwa mashtaka yanayohusiana na maandamano ya 2022-2023, wakili wake ameliambia gazeti la Iran la Sharq Jumatano.

Salehi katika nyimbo zake, aliunga mkono maandamano ya miezi kadhaa nchini Iran mwaka 2022, yaliyochochewa na kifo cha Mahsa Amini, mwanamke mwenye umri wa miaka 22, kilichotokea akiwa chini ya ulinzi wa polisi. Amini alikamatwa kwa madai alivaa hijab isivyofaa.

Salehi alikamatwa mwezi Oktoba 2022 baada ya kutoa taarifa hadharani kuunga mkono maandamano ya nchi nzima.

Alihukumiwa kifungo cha miaka sita na miezi mitatu jela, lakini aliepuka hukumu ya kifo kutokana na uamuzi wa Mahakama ya juu.

Forum

XS
SM
MD
LG