Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 20, 2024 Local time: 05:22

Mgao wa chakula kupunguzwa hadi asilimia 50 kwa wakimbizi 200,000 nchini Tanzania-WFP


Wakimbizi kutoka Burundi waliokimbia machafuko na mvutano wa kisiasa waonekana kwenye kambi ya wakimbizi ya Nyarugusi magharibi mwa Tanzania, Mei 28, 2015.
Wakimbizi kutoka Burundi waliokimbia machafuko na mvutano wa kisiasa waonekana kwenye kambi ya wakimbizi ya Nyarugusi magharibi mwa Tanzania, Mei 28, 2015.

Shirika la mpango wa chakula duniani (WFP) Jumanne limesema kwamba zaidi ya wakimbizi 200, 000 nchini Tanzania watapewa tu nusu ya mgao wa chakula kuanzia mwezi ujao kutokana na ukosefu wa fedha za wafadhili.

Kupunguzwa kwa mgao wa chakula kwa mara ya pili nchini Tanzania katika miezi ya hivi karibuni, kunafuatia hatua kama hizo kote duniani huku shirika hilo la Umoja wa mataifa la chakula likikabiliwa na upungufu wa pesa taslimu na kupanda kwa bei ya chakula, hasa kutokana na vita vya Ukraine.

Mgao wa chakula kwa wakimbizi nchini Tanzania ambao asilimia 70 ni kutoka Burundi na wengine kutoka DRC umepunguzwa kwa kiasi kikubwa tangu mwaka wa 2020, WFP imesema katika taarifa.

“Mwezi Juni, mgao wa chakula utapunguzwa zaidi hadi asilimia 50, hali ambayo itapelekea maelfu ya wakimbizi kukabiliwa na kukidhi mahitaji yao ya lishe,” WFP imesema, ikiongeza kuwa dola milioni 21 zinahitajika kwa haraka ili kuepuka kupunguza zaidi mgao wa chakula.

Forum

XS
SM
MD
LG