Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 20, 2024 Local time: 06:43

Kamanda mkuu wa jeshi la jumuiya ya Afrika mashariki nchini DRC amejiuzulu


Meja Generali Jeff Nyagah, kamanda wa jeshi la jumuiya ya Afrika mashariki akihutubia waandishi wa habari mjini Goma, Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. Nov. 16, 2022. AFP
Meja Generali Jeff Nyagah, kamanda wa jeshi la jumuiya ya Afrika mashariki akihutubia waandishi wa habari mjini Goma, Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. Nov. 16, 2022. AFP

Kamanda wa jeshi la jumuiya ya Afrika mshariki Meja Generali Jeff Nyagah amejiuzulu nafasi hiyo na kurudi Nairobi.

Nyagah ameandika barua kwa uongozi mkuu wa jumuiya ya Afrika mashariki akitoa sababu zake za kujiuzulu, akieleza kwamba usalama wake umekuwa katika hali ya hatari nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na kuathiri utendakazi wake.

Amedai kwamba kuna mikakati inayoonekana baina ya kuathiri utendakazi wa jeshi la jumuiya ya Afrika mashariki. Hajataja wahusika.

Barua hiyo imeandikwa moja kwa moja kwa katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika mashariki.

Ameripoti kwa katibu mkuu kwamba kumekuwepo juhudi za kuchunguza mahali alipokuwa akiishi, ikiwemo kuweka kamera za siri kumchunguza, pamoja na ndege zisizokuwa na rubani kupaa sehemu anayoishi na kufuatilia oparesheni za kikosi chake cha jeshi.

Amesema kwamba juhudi hizo zilianza mapema mwezi Januari 2023.

Meja Generli Nyagah vile vile amesema kwamba kuna kampeni katika vyombo vya habari dhidi ya kikosi cha jeshi la jumuiya ya Afrika mashariki, zinazodai kwamba wanajeshi hao wanashirikian na waasi w M23 badala ya kuwapiga na kuwamaliza nguvu.

Barua ya Nyagah amedai kwamba serikali ya Jamhuri y kidemokrasia ya Congo, imekuwa ikitaka uongozi wa jeshi la jumuiya ya Afrika mashariki uwe wa kupokezana, kinyume na ilivyo katika makubaliano ya jumuiya ya Afrika mashariki.

Amesema kwamba jumuiya ya Afrika mashariki vile vile inaonekana kutompa msaada anaohitaji, ikiwemo kufunga ukurasa wa facebook wa jeshi hilo, akidai kwamba ni mojawapo ya juhudi zisizo za moja kwa moja kufadhisha kazi ya jeshi la jumuiya ya Afrika mashariki.

Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imekosa kutoa pesa kwa ajili ya kufanikisha kazi ya jeshi la jumuiya ya Afrika mashariki, ikiwemo kulipia gharama za makao makuu ya jeshi hilo, umeme, na mishahara kwa wafanyakazi wa kiraia wanaofanya kazi katika makao makuu ya jeshi hilo, ilivyo katika makubaliano ya jumuiya ya Afrika mashariki.

Meja Generali Jeff Nyagah, amesisitiza kwamba hana uhakika na usalama wake na kwa hivyo hawezi kuendelea kuongoza jeshi la jumuiya ya Afrika mashariki nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

XS
SM
MD
LG