Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 12, 2024 Local time: 13:52

Kagame, Sunak wasema waomba hifadhi watahamishwa karibuni


Rais wa Rwanda Paul Kagame na Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak walipokutana mjini London tarehe 9, Aprili, 2024.
Rais wa Rwanda Paul Kagame na Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak walipokutana mjini London tarehe 9, Aprili, 2024.

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak, na Rais wa Rwanda Paul Kagame, wamesema  wanatazamia safari za ndege, chini ya mpango wa Uingereza wa kuwahamishia waomba hifadhi nchini Rwanda zitaanza majira ya machipuko yani Spring.

Kufuatia mkutano kati ya Sunak na Kagame mjini London, ofisi ya Sunak ilisema: "Viongozi wote wawili walitazamia safari za ndege kuelekea Rwanda katika majira ya machipuko."

Waraka uliotolewa kufuatia mkutano kati ya viongozi hao wawili ulieleza kwamba wote walikuwa na matumaini ya kufanikiwa kwa mpango huo licha ya kukabiliwa na vizingiti kadhaa katika miezi ya karibuni.

Kabla ya ndege yoyote kuondoka, serikali ya Uingereza inahitaji kupitisha sheria mpya ambayo Sunak anatumai itafungua njia kwa serikali yake kutuma waomba hifadhi wanaofika Uingereza bila kibali, kwa nchi hiyo ya Afrika mashariki.

Sunak anataka kuwahamisha maelfu ya waomba hifadhi wanaofika Uingereza kwa boti ndogo kila mwaka hadi Rwanda, lakini changamoto za kisheria hadi sasa zimezuia mtu yeyote kupelekwa huko.

Sheria inayolenga kuzuia changamoto zaidi za mahakama kwa mpango huo, itajadiliwa tena bungeni Aprili 15.

Sunak alisema hapo awali anatarajia safari za kwanza za ndege kuondoka kabla ya uchaguzi wa kitaifa unaotarajiwa katika nusu ya pili ya mwaka huu.

Forum

XS
SM
MD
LG