Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 19, 2024 Local time: 20:53

Juhudi za uokoaji zaendelea Afrika Kusini baada ya gorofa kuporomoka


Waokoaji wakiwa katika eneo la jengo lililoporomoka huko George, Mei 7, 2024. Willie van Tonder / AFP.
Waokoaji wakiwa katika eneo la jengo lililoporomoka huko George, Mei 7, 2024. Willie van Tonder / AFP.

Waokoaji walikuwa wakitafuta waathiriwa kwenye vifusi vya jengo la ghorofa tano katika mji wa George huko Afrika Kusini lililoporomoka siku ya Jumanne

Waokoaji wamesema wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuwa wamewasiliana na watu 11 waliokwama kwenye vifusi vya jengo hilo lililokuwa likijengwa na kuua watu watano na 50 bado hawajapatikana.

Colin Deiner, mkuu wa usimamizi wa maafa katika Jimbo la Western Cape, alisema walikuwa wakilenga maeneo ambayo wamekuwa wakisikia sauti za watu.

Maafisa wa mji huo wamesema wafanyakazi 75 wa ujenzi walikuwa kwenye eneo la jengo hilo lilipoporomoka kwa sababu zisizojulikana siku ya Jumatatu.

Rais Cyril Ramaphosa ametoa salamu za rambirambi kwa familia za waliofariki kwenye mkasa huo na kuamuru uchunguzi ufanyike.

Forum

XS
SM
MD
LG