Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 12, 2024 Local time: 13:03

Dangote kufungua ofisi ya mauzo ya bidhaa za mafuta mjini London


Tajiri mkubwa sana wa Nigeria Aliko Dangote.
Tajiri mkubwa sana wa Nigeria Aliko Dangote.

Tajiri mkubwa sana barani Afrika kutoka Nigeria Aliko Dangote, anapanga kufungua ofisi ya mauzo ya bidhaa za mafuta, ikitarajiwa huenda ikafunguliwa h mjini London, ili kusaidia kuendesha  soko la mafuta na bidhaa kutoka kwenye kiwanda chake kipya cha kusafisha mafuta.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, taarifa hiyo ya Jumanne, ni kutoka kwa vyanzo 6 vyenye ufahamu wa kina wa suala hilo. Hatua hiyo itapunguza jukumu la makampuni makubwa ya kimataifa ya mafuta, ambayo kwa miezi kadhaa yamekuwa yakishauriana kuhusu kupeleka mafuta ghafi kwenye kiwanda hicho, pamoja na ufadhili wa kifedha, kwa mabadilishano ya bidhaa za mafuta.

Kiwanda hicho chenye uwezo wa kusafisha mapipa 650,000 kwa siku, kinatarajiwa kutikisa soko la kimataifa la mafuta. Dangote ambaye utajiri wake umeripotiwa kuwa wenye thamani ya takriban dola bilioni 12.7 za kimarekani kulingana na jarida la Forbes, bado hajajibu chochote kuhusu maombi kadhaa yanayomtaka atoe maoni yake.

Makampuni ya mafuta ya BP, Trafigura na Vitol, ni miongoni mwa kadhaa ambayo yamefanya vikao na Dangote mjini Lagosna London katika wiki za karibuni, yakionyesha ari ya kutoa mkopo wa dola bilioni 3 zinazohitajika kuendesha kiwanda hicho.

Forum

XS
SM
MD
LG