Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 08:02

Benki kuu Nigeria yadai kugundua madai ya uongo ya fedha za kigeni dola billioni 2.4


Muonekano wa Makao makuu ya Benki Kuu ya Nigeria huko Abuja, Nov. 11, 2011. Picha na AP
Muonekano wa Makao makuu ya Benki Kuu ya Nigeria huko Abuja, Nov. 11, 2011. Picha na AP

Benki Kuu ya Nigeria imesema wiki hii iligundua dola bilioni 2.4 katika madai ya uongo ya fedha za kigeni baada ya kuchunguza malimbikizo ya dola bilioni 7 zinazopaswa kufutwa.

Mamlaka imesema ugunduzi huo utapunguza mashinikizo yaliyosababishwa na uhaba wa fedha za kigeni na kuonya kwamba madai ya uongo huenda yakaumiza uchumi wa Nigeria.

Ugunduzi wa madai ya uongo yalifuatiwa na ukaguzi wa kina wa mahakama uliofanywa na kampuni ya ushauri ya Deloitte kwa niaba ya Benki Kuu ya Nigeria (CBN).

CBN imeelezea ugunduzi huo wa kushangaza na kusema makosa ni pamoja na nyaraka haramu, kutokuwepo kwa wadai na katika baadhi ya kesi, walengwa walipokea mgao wa fedha za kigeni ambao haukuidhinishwa.

Benki pia imesema baadhi ya wadai walipokea zaidi ya kiwango ambacho waliomba awali.

Gavana wa CBN Olayemi Cardoso amesema benki hautaheshimu miamala batili.

Mchambuzi wa uchumi Ogho Okiti anasema ni hatua yenye mwelekeo sahihi.

“Tunaelekea katika mwelekeo sahihi. Hasa kutokana na kile tulichonacho sasa, kiasi cha asilimia 50 zimeshughulikiwa na tuna kiasi cha asilimia 50 ambazo zitapelekwa.” Alisema Okiti.

“Na hilo likifanyika, linapaswa kusaidia au kuboresha hali yetu ya kifedha. Nadhani yeyote atakayebainika kufanya makusudi na kubuni kutaka kuilaghai Benki Kuu, nadhani wanapaswa kuwajibika kwa hilo.” Aliongeza

Ni mara ya kwanza katika miaka saba kwamba akaunti ambazo zimekaguliwa za CBN matokeo yake yametolewa hadharani.

Nigeria imekuwa ikipambana na uhaba mkubwa wa muda mrefu wa fedha za kigeni ambao umechelewesha maendeleo ya uchumi, kushuka thamani kwa sarafu na hali imekuwa mbaya sana ya mfumuko wa bei.

Mamlaka zinasema ukaguzi umekuwa ni muhimu ili kuweza kuelewa matatizo na benki kuu na uchumi.

CBN hadi sasa imelipa kiasi cha dola bilioni 2.3 katika madai halali, ikiwemo fedha ambazo zinadaiwa na mashirika ya ndege, sekta za uzalishaji na nishati.

Mchumi na mkurugenzi katika Center for Social Justice Eze Onyekpere anasema ukaguzi hautarekebisha uchumi mbaya wa Nigeria.

“Kuna madeni mengine. Haitasuluhisha chochote. Msimamo wa sarafu katika misingi ya thamani ni mbali ya CBN na sera zake za fedha. Yote haya ni kuhusu muundo wa utawala iwe katika eneo la kifedha, kiviwanda,” alisema

“Elimu na sera za afya. Umesikia gavana wa CBN amewaambia wawakilishi katika bunge kwamba utalii wa kiafya na malipo ya ada za shule yalichukua kiasi cha dola bilioni 40 ndani ya kipindi cha miaka 10, hiyo ni sawa na dola bilioni 4 kwa mwaka.” Alisema Onyekpere.

Hata hivyo, Onyekpere anasema ugunduzi wa ukaguzi unaashiria matatizo makubwa ndani ya mfumo wa fedha za kigeni Nigeria na lazima walizungumzie suala hilo.

“Jumuiya ya madola, fedha za kigeni, rasilimali za Nigeria hazikushughulikiwa vizuri. Katika miaka kadhaa zimeibiwa kimfumo. Hali ya sasa ya uchumi tunayojikuta ni matokeo ya wizi wa moja kwa moja.”alisema Onyekpere.

Alipochukua madaraka mwaka jana, Rais Bola Tinubu aliahidi kufanya msako mkali kwa rushwa na kupitisha sheria za mageuzi ili kuboresha uchumi. Kwahiyo hadi sasa, uchumi haujakaa vizuri na wanigeria bado wako katika hali ya kukaa na kusubiri.

Forum

XS
SM
MD
LG