Wizara ya Afya ya Ukanda wa Gaza imesema watu zaidi ya 32,000 wameuawa wakati wa mashambulizi ya Israel
China iliweka ushuru kwa mvinyo wa Australia mwaka 2020 wakati wa mzozo wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili
Rais Mahmoud Abbas alimteua Mohammad Mustafa, mshauri wa muda mrefu kuwa Waziri Mkuu wa Palestina mapema mwezi huu.
Chama cha Kejriwal cha Aam Aadmi Party (AAP) kinasema kesi hiyo imetungwa na ina ushawishi wa kisiasa
Rais wa Russia Vladimir Putin amewaonya washirika wa Ukraine, mataifa ya Magharibi, dhidi ya kutoa msaada wa vituo vya anga katika nchi zao.
UN inasema vita vya magenge vimeongezeka wakati wapinzani wenye silaha wakijihusisha na wimbi jipya la mashambulizi
Russia ilisema Jumatano imezuia mashambulizi ya roketi yaliofanywa na Ukraine yakiulenga mkoa wa Belgorod, wakati Ukraine ilisema Russia imeishambulia usiku kucha kwa droni 13.
Makamu wa rais mteule wa Taiwan Hsiao Bi-Khim amekamilisha ziara yake ya kidiplomasia ya Ulaya wiki iliyopita, suala ambalo limekera Beijing, wakati akisimama kwenye mataifa matatu pamoja na kukutana na wanasiasa kadhaa mjini Brussels.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema Jumatano kwamba haiungi mkono mpango wa Pakistan kujenga bomba la kusafirisha gesi kutoka Iran. Msemaji wa wizara hiyo Mathew Miller hata hivyo alikataa kutoa taarifa za kina kuhusu suala hilo.
Wanamgambo wa Hezbollah wa Lebanon, Jumatano wamefanya mashambulizi ya roketi kaskazini mwa Isreal, wakijibu mashambulizi ya anga ya Israel yaliyouwa watu 7 kusini mwa Lebanon.
Mahakama moja ya Russia imeongeza muda wa kukaa kizuizini kabla ya kusikilizwa kesi ya mwanahabari wa Marekani Evan Gershkovich, ambaye alikamatwa karibu mwaka mmoja uliopita kwa tuhuma za ujasusi zinazochukuliwa kwa sehemu kubwa ni uongo
Timu za kutafuta na kuokoa zinawatafuta karibu watu 20 ambao hawajulikani walipoa baada ya daraja kubwa kuporomoka katika mji wa Baltimore, Maryland Marekani.
Pandisha zaidi