Rais wa Kenya William Ruto Alhamisi jioni alitangaza kifo cha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Francis Ogolla, kilichotokana na ajali ya helikopta iliyotokea majira ya alasiri Kaskazini Magharibi mwa nchi.
Seneta wa Marekani Chris Coons alipongeza Baraza la Seneti kwa kupitisha kwa kauli moja azimio lake ambalo linalaani rekodi ya haki za binadamu ya serikali ya Eswatini na mauaji ya mwanaharakati wa haki za binadamu wa Eswatini Thulani Maseko.
Marekani imewazuia maafisa wanne wa zamani wa serikali ya Malawi kuingia nchini, kwa sababu ya kuhusika kwao katika ufisadi mkubwa, Wizara ya Mambo ya Nje ilisema Jumatano.
Baraza la Seneti la Marekani limepiga kura ya kutupilia mbali vifungu vyote vya mashtaka dhidi ya waziri wa Usalama wa Ndani, Alejandro Mayorkas, na kumaliza kesi yake, kuhusiana na jinsi alivyoshughulikia mpaka wa Marekani na Mexico.
Kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia maswala ya haki za binadamu, Volker Turk amezitembelea kambi za watu waliokoseshwa makazi kaskazini mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Waziri Mkuu wa Qatar na Waziri wa Mambo ya Nje, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al thani amesema leo kuwa mashauriano kwa sitisho jipya la mapigano huko Gaza yako katika ‘awamu nyeti.’
Kombora la Russia Jumatano liliua wakazi 9 na kuharibu majengo na miundombinu ya mji wa kaskazini mwa Ukraine wa Chernihiv, maafisa wa mji huo walisema.
Mapigano kati ya jeshi la Sudan na kikosi hasimu cha wanamgambo yaliua raia 25 katika mji wa kaskazini mwa Darfur wa El-Fasher, kundi la wanasheria wanaotetea demokrasia lilisema Jumanne.
Waziri wa Ulinzi wa Israel alisema Jumanne vitisho vya Iran havitazuia taifa lake kujibu mashambulizi ya anga ya Jumapili dhidi ya taifa hilo la Kiyahudi.
Mkutano wa ngazi ya juu wa kuahidi misaada kwa Ethiopia, uliofadhiliwa na Ethiopia, Uingereza, na Umoja wa Mataifa ulipokea karibu dola milioni 628.9 kama msaada wa kibinadamu wa kuokoa maisha kwa mamilioni ya raia wa nchi hiyo wanaoteseka.
Pentagon imesema Lloyd Austin na Admirali Dong Jun wa China walijadili uhusiano wa ulinzi na masuala ya usalama wa kimataifa
Pandisha zaidi