Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 20:54

Wakristo washerehekea siku kuu ya kufufuka kwa Yesu


Wakristo wakibeba misalaba katika njia ya Dolorosa siku ya Ijumaa Kuu mjini Jerusalem. Aprili18, 2014
Wakristo wakibeba misalaba katika njia ya Dolorosa siku ya Ijumaa Kuu mjini Jerusalem. Aprili18, 2014

Waumini wa dini ya Kikristo walikusanyika kwenye kaburi la kale lililo wazi ,ambalo limekatwa kutoka kwenye jabali wakiimba nyimbo zikilezea “Yesu amefufuka"

Wakristo duniani kote wanasherehekea Siku kuu ya kufufuka kwa Yesu Kristo kutoka kwa wafu huku kukiwa na ibada maalum jijini Jerusalem, jiji ambalo kwa mujibu wa kitabu kitakatifu cha Biblia, matukio hayo yalifanyika.

Ibada hiyo ilifanyika katika katika Garden Tomb, eneo ambalo linafanana na mahala ambapo Biblia inaelezea Yesu Kristo alizikwa. Waumini wa dini ya Kikristo walikusanyika kwenye kaburi la kale, lililo wazi ambalo limekatwa kutoka kwenye jabali wakiimba nyimbo zikilezea “Yesu amefufuka.”

Makasisi na watawa wengine wakiwa wamevalia kanzu kwa ajili ya sherehe hizo za kidini walisoma kutoka vitabu vya Biblia vinavyoelezea kuhusu matukio hayo huku moshi uliohanikiza ukipaa juu ya kaburi hilo wazi la kale, ambako Wakristo wanaamini ni mahali mahsusi alipofufuka Yesu kutoka kwa wafu.

Kulikuwa na waumini wengi kutoka nchi mbalimbali za dunia kwa sababu kalenda za waumini wa Kikristo kutoka madhehebu ya Orthodox na yale ya Magharibi iliwiana mwaka huu na hivyo kusherehekea siku kuu hiyo kwa pamoja
XS
SM
MD
LG