Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 00:07

Volcano yalipuka Chile


Majivu kutoka kwa volcano yanaonekana angani kutoka eneo la Calbuco nchini Chile.
Majivu kutoka kwa volcano yanaonekana angani kutoka eneo la Calbuco nchini Chile.

Mlipuko wa volcano kwenye mlima wa Calbuco kusini mwa Chile umetokea mara mbili katika kipindi cha saa 24 na kuacha eneo hilo katika hali ya taharuki. Volcano hiyo ililipuka kwa mara ya kwanza Jumatano baada ya kipindi cha zaidi ya miongo minne na kutupa majivu ya urefu wa kilomita 10 angani.

Mamlaka ya Chile yaliyoshtushwa na tukio hilo yalianza kuwaondoa maelfu ya watu kutoka eneo hilo na kutoa ilani kwa miji ya Puerto Montt na Puerto Varas, ambayo ni maarufu kwa utalii. Mlipuko mwingine ulishuhudiwa mapema Alhamisi.

Hakuna majeruhi yaliyoripotiwa. Mamlaka yameondoa zaidi ya watu 4000 huku gesi na majivu zikiendelea kutoka kwenye volcano hiyo. Idara ya kitaifa ya masuala ya jiolojia na Madini nchini Chile imeonya huenda mlipuko wa tatu ukatokea.

XS
SM
MD
LG