Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 19:05

Mvutano kati ya Ukraine na Russia waendelea


Wanaharakati wa Ukraine nje ya wizara ya maswala ya ndani mjini Kyiv, Aprili 14, 2014
Wanaharakati wa Ukraine nje ya wizara ya maswala ya ndani mjini Kyiv, Aprili 14, 2014

Rais wa Marekani Barack Obama alimwonya Rais wa Russia Vladmir Putin katika mazungumzo kwa njia ya simu kuwa Moscow itakabiliwa na gharama zaidi ikiwa hatua zake huko Ukraine zitaongezeka.

Waandamanaji wanaounga mkono Russia hapo Jumatau walikaidi tarehe ya mwisho ya serikali ya kuyaachia majengo walinashikilia ili wapewe msamaha, huku kaimu rais wa Ukraine akitishia kutumia majeshi kuwadhibiti.

Dazeni ya waandamanaji walivunja madirisha kwenye makao makuu ya polisi huko mashariki mwa mji wa Horlivka na kuwafunga pingu polisi wakati walipochukua udhibiti wa majengo hayo.

Rais wa Marekani Barack Obama alimwonya Rais wa Russia Vladmir Putin katika mazungumzo kwa njia ya simu Jumatatu kuwa Moscow itakabiliwa na gharama zaidi ikiwa hatua zake huko Ukraine zitaongezeka.

Pia alimsihi kiongozi huyo wa Russia kutumia ushawishi wake kuwarai waandamanaji waondoke kwenye majengo wanayoshikilia. Naye rais Putin alimsihi rais Obama kuiomba serikali ya Ukraine kutotumia nguvu dhidi ya waandamanaji.
XS
SM
MD
LG