Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 12:54

Marekani kupeleka wanajeshi Afrika magharibi kupambana na Ebola


Mataifa yaliokumbwa na Ebola katika Afrika magharibi, Agosti 30, 2014
Mataifa yaliokumbwa na Ebola katika Afrika magharibi, Agosti 30, 2014

Rais Barack Obama atatangaza juhudi za Marekani za kusaidia nchi za Afrika Magharibi kupambana na ugonjwa hatari wa Ebola. Bwana Obama atatangaza mpango wa kupeleka wanajeshi 3,000 huko Afrika Magharibi Jumanne jioni akiwa katika taasisi ya kudhibiti na kuzuia magonjwa nchini Marekani-CDC mjini Atlanta , Georgia.

Wanajeshi hao watajenga vituo 17 vya afya na kila kituo kitakuwa na vitanda 100 ili kuweza kuwatenga na kutibu walioambukizwa kirusi cha ugonjwa wa Ebola.

Ujumbe huo wa Marekani pia utajenga kituo cha kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa afya 500 kwa wiki. Kwa mujibu wa taarifa kutoka White House kituo cha usimamizi wa shughuli hiyo kitakuwa katika mji mkuu wa Liberia, Monrovia.

Wakati huo huo baraza la usalama la Umoja wa Mataifa litafanya kikao cha dharura Alhamis kuzungumzia ugonjwa huo. Balozi wa Marekani katika Umoja wa mataifa, Samantha Power alisema ugonjwa huo ni hatari kwa jumuiya ya kimataifa na ni lazima dunia ishirikishwe kupambana nao.

Valerie Amos
Valerie Amos

Nao maafisa wa shirika la afya Duniani-WHO walisema mataifa ya magharibi yaliyokumbwa na ugonjwa wa Ebola yako katika ukingo wa mgogoro mkubwa wa kibinadamu kama hayatapatiwa msaada karibuni.

Mratibu wa misaada ya dharura katika WHO, Valerie Amos alisema akiwa huko Geneva kuwa nchi ya Liberia na Sierra Leone bado zinajaribu kujikwamua kutokana na migogoro ya kibinadamu iliyotokea chini ya muongo mmoja uliopita na nchi ya Guinea ndio kwanza inajikwamua kutoka katika mgogoro wa kisiasa.

XS
SM
MD
LG