Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 03:51

Kerry aongoza juhudi za kupambana na kundi la Islamic State


Viongozi kwenye mkutano wa Paris uliojadili namna ya kukabiliana na kundi la Islamic State, Sept 15, 2014
Viongozi kwenye mkutano wa Paris uliojadili namna ya kukabiliana na kundi la Islamic State, Sept 15, 2014

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry anaendelea na juhudi za kujenga ushirika unao-ongozwa na Marekani dhidi ya kundi la wanamgambo wa Islamic State kwenye mkutano wa Jumatatu mjini Paris ambao unawakutanisha wanadiplomasia kutoka nchi 26, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na jumuiya ya nchi za kiarabu-Arab League.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande na Rais wa Iraq Fouad Massoum ni wenyeji wa mkutano unaolenga juu ya amani na usalama nchini Iraq ambako wanamgambo wa Islamic State wanadhibiti maeneo mengi katika sehemu za kaskazini na magharibi mwa nchi hiyo.

Kerry alisema Jumapili kwamba nchi kadhaa ziko tayari kujiunga katika mapambano ikiwemo nchi za mashariki ya kati na kwingineko zinatoa msaada wa kijeshi na kufanya mashambulizi ya anga kama ikibidi.

Rais wa Ufarans Francois Hollande (R) na Rais wa Iraq Fouad Massoum
Rais wa Ufarans Francois Hollande (R) na Rais wa Iraq Fouad Massoum

Lakini Rais wa Iraq massoum aliliambia shirika la habari la Associated Press kwamba sio muhimu kwa mataifa ya kiarabu kufanya mashambulizi ya anga akisema kile kinachohitajika ni wao kushiriki katika maamuzi ya kwenye mkutano.

Alielezea umuhimu wa kuchukua hatua dhidi ya kundi la Islamic State akisema ni kwa maslahi ya kila mmoja.

Iran sio moja ya nchi 26 zinazohudhuria katika mkutano. Bwana Massoum alisema anafikiri Iran ingealikwa hasa ikizingatiwa kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakishirikiana mpaka na Irak na msaada wa kibinadamu ambao Iran imetoa wakati wa mgogoro.

Pia jumapili Waziri Mkuu wa Australia Tony Abott alisema nchi yake karibuni itapeleka wanajeshi 600 na ndege kadhaa za kivita katika eneo hilo ikiwa ni kujibu ombi rasmi kutoka Marekani kwa msaada wa kimataifa.

XS
SM
MD
LG