Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 23:53

Obama atangaza mageuzi muhimu ya uhamiaji


Rais Obama alihutubia taifa juu ya mageuzi ya uhamiaji, Nov 20, 2014.
Rais Obama alihutubia taifa juu ya mageuzi ya uhamiaji, Nov 20, 2014.

Akilihutubia taifa kutokea White House Alhamisi usiku rais Obama alisema hatua yake haitobadili sheria ya uhamiaji kwa wakati huu bali alitowa wito kwa wabunge wanaopinga hatua yake kupitisha sheria ambayo itarekebisha matatizo yaliyopo katika mfumo wa uhamaiji ambao umeharibika.

"Ninaendelea kuamini kwamba njia bora ya kutanzua tatizo hili ni kufanya kazi pamoja kupitisha sheria zinazostahiki, kwa hivyo hadi itakapotendeka mimi nina haki za kisheria kuchukua uamuzi kama walivyochukua marais walonitangulia Wademcorat na Warepublican, utakaosaidia kufanya mfumo wetu wa uhamiaji uwe wa haki na wenye usawa."

please wait

No media source currently available

0:00 0:04:55 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Rais obama anasema kutokana na hali hiyo ataamrisha hatua zifuatazo kuchukuliwa.

"Tunapendekeza mpango ufuatao, ikiwa umeishi Marekani kwa zaidi ya miaka mitano, ikiwa una watoto ambao ni raia wa Marekani au ni wakazi mwenye hati za halali, ikiwa utajiandikisha na kuchunguzwa ukawa hujatenda uhalifu na kulipa mchango wako wa haki wa kodi , basi utaweza kuomba kuishi katika nchi hii kwa muda bila ya hofu ya kurudishwa nyumbani na utoke mafichoni.

Wahamiaji wasio halali kutoka Guatemala wakiondolewa Marekani
Wahamiaji wasio halali kutoka Guatemala wakiondolewa Marekani

Rais Obama anasema mabadiliko haya hayatawahusu waloingia hapa nchini karibuni, au watakaoingia Marekani kinyume cha sheria katika siku za baadae, mpango hautowapatia haki ya kuwa raia na hauwapati watu haki sawa na raia kwani, anasema hilo ni jukumu la bunge kuamua.

Wabunge wa chama cha Republican wameshasema ikiwa rais amechukua hatua hiyo watalazimika kuchukua hatua za kupinga mipango yake au hata kufikisha mashtaka mahakamani kwani wanaamini anakwenda kinyume cha sheria.

Hata hivyo wakili wa uhamiaji na naibu wa chama cha Mawakili wa Uhamiaji Marekani Bi. Naima Said anasema hatua hizo za rais zinafuatana na sheria.

Bi. said anasema hatua zilizochukuliwa na Rais Obama ni miongoni mwa mambo walokuwa wakitetea kwa muda mrefu na kwamba upinzani wa wabunge wa chama cha Republican ni mkakati wa kisiasa kwani wanadhani kutangazwa kwa amri hiyo ya rais inampatia Rais Obama nguvu miongoni mwa wahamiaji.

XS
SM
MD
LG